Skip to product information
 +153 Reviews (4.75)

PowerSquare flat solar work light with a built-in 4000mAh power bank

PowerSquare flat solar work light with a built-in 4000mAh power bank

HOT PRODUCT | LOW STOCK

Mwanga wa chumba kizima. Chaji ya simu yako.

  • 💡Umeme ukikatika, chumba kizima kinang'aa. 
  • 🔋Inachaji simu yako pia. 
  • ☀️Ichaji kwa jua au USB-C. 
  • 🧲Isimamishe, ining'inize, ibebe au ibandike. 
  • 🚚Delivery bure. Lipa ukipokea. 

✓ AfrickanTZ · Dar: ndani ya saa 24 · Mikoani: saa 48

Order Via WhatsApp View full details
Ione ikifanya kazi

Taa moja. Kazi sita.

Hakuna maigizo ya studio. Hii ni taa halisi, ikifanya kazi za kila siku.

Giza totoro, PowerSquare inawashwa kwa sekunde moja Simu ikichajiwa na power bank ya PowerSquare PowerSquare ikibadilisha rangi 3 za mwanga PowerSquare ikinasa kwenye friji kwa sumaku Sola nyuma ya PowerSquare ikichaji kwa jua Taa za kijani zikionyesha chaji iliyobaki
Mkono ukibonyeza PowerSquare, chumba chenye giza kinang'aa
Mgao wa umeme ukifika

Umeme umekatika. Simu iko 3%.

Unaijua hii hali. Umeme unakatika mkiwa mnakula. Unachukua simu uwashe tochi, betri tayari iko nyekundu.

Sasa una matatizo mawili: hakuna mwanga, na simu inakaribia kuzima. Hakuna simu, hakuna M-Pesa, hakuna WhatsApp.

PowerSquare inatatua yote mawili kwa mara moja.

💡 Mwanga wa chumba kizimaPaneli nzima ya LED inaangaza chumba chote, si kona moja tu.
🔋 Chaji ya simu yakoChomeka simu kwenye taa, inaanza kuchaji papo hapo.
PowerSquare ikiwaka na kuchaji simu kwa power bank yake
Taa moja. Kazi mbili.

Taa na power bank.

Ndani ya PowerSquare kuna betri ya 4000mAh. Inawasha taa, na kupitia mlango wa USB inachaji simu yako. Kifaa kimoja badala ya viwili, na jua linaijaza bure.

  • ✓Tumia waya wako wa kawaida wa simu. Chomeka kwenye mlango wa USB, simu inaanza kuchaji.
  • ✓Simu, M-Pesa, WhatsApp: simu yako inapata chaji hata giza likiingia.
  • ✓Ijaze kwa jua au USB-C, iko tayari kwa mgao ujao.
Simamisha. Ning'iniza. Beba. Bandika.

Mwanga pale unapouhitaji.

Mshikio wa kukunja na sumaku zilizomo ndani: hutashika tochi kwa meno tena.

PowerSquare imesimamishwa, imening'inizwa, inabebwa na imebandikwa kwenye chuma
01 IsimamisheKunjua mshikio wake, elekeza mwanga pale unapotaka.
02 Ining'inizeKwenye msumari, kamba au ndoano ya darini.
03 IbebeShika mshikio wake, nenda getini, chooni au shambani.
04 IbandikeSumaku zinaishika kwenye gari, friji au mlango wa chuma. Mikono yote miwili huru.
🏠 Nyumbani mgao ukifika🏪 Duka na genge usiku🍲 Mama lishe🔧 Mafundi na madereva📚 Wanafunzi kujisomea⛺ Safari na kambi
PowerSquare inachaji kwa sola au kwa USB-C
Chaji kwa njia yako

Jua mchana. USB-C kukiwa na mawingu.

  1. 1Iache juani. Sola iliyo nyuma inachaji betri bure, kila siku.
  2. 2Wiki ya mawingu? Ichomeke kwenye chaja yoyote ya simu au power bank kwa waya wa USB-C.
  3. 3Angalia taa 4 za kijani. Zinaonyesha chaji iliyobaki, kwa hiyo mgao haukushtui tena.
Jinsi ya kuagiza

Kutoka kuagiza mpaka mwanga, hatua 3 tu.

  1. 01
    Agiza kwa WhatsApp au fomuTuambie jina lako, mahali ulipo na unataka taa ngapi.
  2. 02
    TunakuthibitishiaTunakupigia au kukuandikia WhatsApp kuthibitisha anwani yako.
  3. 03
    Lipa ukipokeaIkague ukiipokea: iwashe, ijaribu, ndipo ulipe. Hakuna malipo ya awali.
Saa 24Delivery Dar es Salaam
Saa 48Delivery mikoani
🚚 BureDelivery mpaka ulipo
💵 UkipokeaHakuna malipo ya awali
Maswali

Una maswali? Tuna majibu.

Kweli inachaji simu yangu?

Ndiyo. Chomeka waya wako wa kawaida wa kuchaji simu kwenye mlango wa USB wa taa. Betri ya 4000mAh inaongeza chaji kwenye simu iliyokaribia kuzima, uendelee kupiga simu, kutumia M-Pesa na WhatsApp.

Sola inafanya kazi siku za mawingu?

Sola inachaji haraka zaidi kwenye jua kali. Siku za mawingu au mvua inachaji polepole, kwa hiyo ichomeke kwenye chaja yoyote ya simu au power bank kwa waya wa USB-C. Njia mbili za kuchaji, hukwami.

Mwanga unadumu muda gani?

Inategemea rangi unayochagua na chaji iliyopo kwenye betri. Taa 4 za kijani juu zinakuonyesha chaji iliyobaki muda wowote, kwa hiyo unajua wakati wa kuichaji.

Mwanga wake ni mkali kiasi gani?

Mbele yote ni paneli ya LED, kwa hiyo inaangaza chumba kizima, si kona moja tu. Chagua nyeupe kali kwa kazi na kusoma, njano ya joto kwa kupumzika, au nyeupe asilia kwa kila siku.

Sumaku zinafanyaje kazi?

Sumaku zinashika taa kwenye chuma tambarare: bodi ya gari, friji, mlango wa chuma au rafu. Iweke kwenye sehemu safi na tambarare ili ishike vizuri, na mikono yako yote miwili ibaki huru kwa kazi.

Ni vigumu kuitumia?

Hapana. Kitufe kimoja kinawasha na kubadilisha rangi. Kunjua mshikio wake uisimamishe, uining'inize au uibebe. Hakuna kufunga nyaya, hakuna fundi.

Kwa nini ninunue mbili?

Moja ya nyumbani, moja ya dukani au ya gari. Ukinunua mbili unapata punguzo la 50%, kwa hiyo kila taa inakuwa nusu bei. Mgao ukifika, nyumba na biashara zote zina mwanga.

Nikipokea, nifanye nini kabla ya kulipa?

Ikague kabla hujalipa. Iwashe, badilisha rangi, chomeka simu uone inachaji. Ukiridhika, ndipo ulipe. Ukiwa na swali lolote baadaye, tuandikie WhatsApp +255 795 588 306 tukusaidie.

Naagizaje? Delivery inachukua muda gani?

Bonyeza kitufe cha WhatsApp au jaza fomu. Tunakupigia au kukuandikia kuthibitisha, kisha tunakuletea. Dar es Salaam mpaka mlangoni ndani ya saa 24, mikoani ndani ya saa 48. Delivery ni bure na unalipa ukipokea.