
Jinsi ya kuagiza
Kuagiza ni rahisi, hatua 3 tu
Hulipi chochote kabla. Unalipa ukishaona bidhaa yako mlangoni.
-
01
Chagua ofa yako
Chagua idadi ya taa unazotaka, kisha bonyeza Agiza.
-
02
Tunakupigia kuthibitisha
Simu au WhatsApp fupi kuthibitisha oda na mahali ulipo.
-
03
Kagua, kisha ulipe
Usafiri ni bure. Kagua bidhaa mlangoni, kisha ulipe.
- Hulipi kabla
- Usafiri bure Tanzania
- Kagua kabla ya kulipa
Maswali yako
Majibu ya wazi, kabla ya kuagiza
+Nahitaji fundi au kutoboa ukuta?
Hapana. Bandika plate ya chuma (ina gundi tayari) kwenye sehemu safi, kavu na tambarare, kisha weka taa: sumaku inaishika papo hapo.
Inachukua chini ya dakika moja. Hakuna waya, hakuna zana.
+Umeme ukikatika, inafanya kazi?
Ndiyo. Haitumii umeme wa nyumba. Inatumia betri yake iliyochajiwa, kwa hiyo inaendelea kuwaka hata umeme ukikatika.
+Betri inadumu muda gani?
Chaji kwa saa 3 hivi. Kwenye hali ya sensor inaweza kusubiri hadi saa 1,200, na ikiwaka mfululizo inawaka saa 9 hadi 15.
Muda halisi unategemea mwangaza na hali uliyochagua. Taa nyekundu: inachaji. Kijani: imejaa.
+Nachaji vipi?
Tumia kebo ya USB-C na chaja yoyote ya simu. Iondoe kwenye sumaku, ichaji, kisha irudishe.
+Itawaka hata mchana?
Ukitaka tu. Kitufe kimoja kina hali 4: inawaka muda wote, sensor ya usiku (inawaka gizani tu), mchana na usiku, na zima.
Bonyeza kitufe cha rangi kubadili njano, asili au nyeupe. Shikilia kupunguza au kuongeza mwanga.
+Naweza kuibandika wapi?
Sehemu safi, kavu na tambarare: mbao, vigae, chuma au plastiki. Chini ya kabati, ndani ya kabati la nguo, ngazini au kwenye korido.
Epuka ukuta wenye mvuke mwingi (karibu na bafu la maji ya moto): gundi ya plate inaweza kulegea. Safisha na kausha sehemu kwanza.
+Ndani ya boksi kuna nini? Nalipaje?
Taa 1 ya sensor (sm 30) na plate 2 za chuma zenye gundi.
Unalipa ukipokea. Hulipi chochote kabla. Tunakupigia kuthibitisha oda, kisha unakagua taa yako na kulipa.


